• Tanzania –Zambia- Kenya zasaini makubaliano ya Usafirisaji Umeme

  Tanzania –Zambia- Kenya zasaini makubaliano ya Usafirisaji Umeme

  Na Teresia Mhagama Nchi za Tanzania, Zambia na Kenya zimetiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa miundombinu ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400. Makubaliano hayo ya awali yamesainiwa tarehe 15 desemba 2014, nchini Zambia na Mawaziri wanaosimamia sekta ya Nishati […]

   
 • Kamishna wa Madini afungua mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake

  Kamishna wa Madini afungua mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake

  Kamishna wa madini nchini, Mhandisi Paul Masanja amefungua rasmi mafunzo ya uongezaji thamani madini kwa wanawake 15 wa kitanzania waliopata ufadhili wa masomo hayo ambayo ni matunda ya  harambee iliyoanzishwa na Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha mwaka 2012. Mafunzo hayo ya ukataji madini yatakayowawezesha […]

   
 • Madini ya Vito yenye thamani ya shilingi bilioni 6.88 yauzwa

  Madini ya Vito yenye thamani ya shilingi bilioni 6.88 yauzwa

  Serikali kuvalia njuga utoroshaji Tanzanite Imeelezwa kuwa madini ya Vito yenye thamani ya shilingi bilioni 6.88 yaliuzwa katika Maonesho ya Pili ya Kimataifa ya Vito- Arusha yaliyofanyika mwaka 2013 na serikali kupata mapato ya jumla ya shilingi milioni 227.4. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava […]

   
 • TMAA yapiga mnada madini yaliyokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi

  TMAA yapiga mnada madini yaliyokamatwa yakitoroshwa nje ya nchi

  Madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliyokamatwa wakati yakisafirishwa nje ya nchi bila kufuata taratibu za nchi za usafirishaji madini yamepigwa mnada na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA). Madini hayo yamepigwa mnada jijini Arusha katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika katika hoteli […]

   
 • Nishati na Madini watakiwa kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi

  Nishati na Madini watakiwa kuboresha tathmini ya mapendekezo ya miradi

  Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini wametakiwa kuboresha ufanyaji wa tathmini ya mapendekezo ya miradi (project proposal) ya Wizara kwa uwazi kwani ina mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Lusius Mwenda, alipokuwa akifunga […]

   
 • Tanesco yakaribisha kampuni makini,zisizoendekeza rushwa

  Tanesco yakaribisha kampuni makini,zisizoendekeza rushwa

  Vipaumbele ni gesi, makaa ya mawe, maji, nishati jadidifu Ili kuhakikisha kuwa asilimia 75 ya watanzania wanatumia umeme ifikapo mwaka 2025, Serikali imeeleza kuwa kampuni yoyote inayotaka kuwekeza katika sekta ya nishati nchini lazima iwe yenye dira na mwelekeo mpya, isifanye kazi katika mazingira ya   rushwa, ubabaishaji, na ijikite katika […]

   
 • Waziri Muhongo akutana na Makamu wa Rais wa MCC

  Waziri Muhongo akutana na Makamu wa Rais wa MCC

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza […]

   
 • Burundi kusafirisha umeme kupitia Tanzania

  Burundi kusafirisha umeme kupitia Tanzania

  Serikali za Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa makubaliano ya kuruhusu Serikali ya Burundi kusafirisha umeme wake wa kutoka Rusumo kupitia Tanzania. Makubaliano hayo yalisainiwa Oktoba 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Migodi wa […]