Home » images »

Dk. Pallangyo akutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Mhandisi  Juliana Pallangyo tarehe 08 Februari, 2017 amekutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo  ya Afrika (AfDB) ambapo Benki hiyo imeonesha nia ya kufadhili  miradi ya kuzalisha  umeme. Miradi hiyo ni pamoja na; Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji wa Kakono (MW 87); Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya maji wa Malagarasi (MW 44.8); Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha wenye msongo wa kV 400 kutoka Mbeya – Sumbawanga- Kigoma na Mradi wa kusambaza umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme mijini (Urban Electrification).

Imeandaliwa na:

Greyson Mwase,

Afisa Habari,

Wizara ya Nishati na Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606

Barua Pepe: info@mem.go.tz                                                                               

Tovuti: mem.go.tz