Hotuba-Mh. Prof. Muhongo uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha kufua umeme Kinyerezi II

 

Kwanza kabisa napenda kukushukuru Mh Rais, kwa kukubali kuja kuweka jiwe la Msingi ili kuanza ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II wa kujenga Mtambo wa kufua umeme wa megawati 240.

Mhe Rais nafahamu kuwa una majukumu mengi ya kiserikali ambayo pia ni muhimu kama hili, lakini kwa uzalendo wako, umekubali kuacha shughuli zingine zote ili uje kukuweka jiwe hili la msingi. Hii ni kuonyesha umuhimu unaouweka katika miradi ya umeme na kwa hili tunakushukuru sana.

Mhe Rais

Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 344 sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Japan.  Serikali ya Japan itatoa asilimia 85 sawa na Dola za Marekani milioni 292 na Mchango wa Serikali ya Tanzania ni Dola za Marekani milioni 52 sawa na asilimia 15 ya mkopo huo na nakushukuru sana Mhe. Rais kwamba kiasi hicho cha dola milioni 52 sawa na pesa za kitanzania Bilioni 110 umezitoa wewe mwenyewe na tayari Mkandarasi ameanza kazi kama unavyoona. Tunakushukuru sana.

Mradi huu wa Kinyerezi (II) wa Megawati 240 utajengwa na Kampuni ya SUMITOMO ya Japan ambayo ni Mkandarasi aliyepatikana kwa utaratibu wa kufanya shughuli zote za Kihandisi, Ununuzi wa mtambo na Kujenga “EPC contractor”.

>>Soma Zaidi>>