Hotuba ya Mkurugenzi wa EWURA Bw. Felix Ngamlagosi kwenye uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa sekta ndogo ya mafuta kwa mwaka 2016

 

Ndugu Mgeni Rasmi

Napenda kutumia fursa hii, kuwakaribisha wote katika mkutano huu ambao lengo lake kubwa ni kuzindua Ripoti ya Utendaji katika sekta ndogo ya Mafuta ya petroli kwa mwaka 2016. Ripoti itakayozinduliwa leo inatoa maelezo ya kina kuhusiana na biashara ya mafuta hapa nchini kwa mwaka 2016. Pia, ripoti imesheheni maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa shughuli na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo takwimu na taarifa muhimu zinazohusiana na masuala ya mafuta ya petrol nchini kwa mwaka 2016.

Ndugu Mgeni Rasmi, huu ni mkutano wa kazi. Kwenye ratiba ya kazi za leo, pamoja na mambo mengine, kwanza utazindua Ripoti ya Utendaji katika Sekta Ndogo ya Mafuta ya Petroli kwa mwaka 2016. Pili, utatunuku vyeti na tuzo kwa baadhi ya watoa huduma, ambao utendaji wao katika tasnia ya biashara ya mafuta nchini katika mwaka 2016 ulionekana kuwa mzuri zaidi. Ripoti ambayo utaizindua hivi punde, ipo katika mtiririko ufuatao:

  1. Sheria, kanuni na taratibu zinazotumika katika usimamizi wa sekta ndogo ya Mafuta ya petroli katika mkondo wa kati na chini ambazo ndizo nyenzo kuu zinazotumika katika utendaji wa EWURA;
  2. Uagizaji, upokeaji na usambazaji wa mafuta ya petroli, hususan utekelezaji wa mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (BPS).
  3. Mwenendo wa bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia na soko la ndani;
  4. Usimamizi wa ubora wa miundombinu ya kupokelea, kuhifadhi na kusambaza mafuta;
  5. Usimamizi wa ubora na usalama wa bidhaa ya mafuta ya petroli;
  6. Utoaji wa leseni kwa ajili ya biashara ya mafuta ya petroli nchini;
  7. Ufuatiliaji wa mwenendo wa ushindani katika soko la mafuta nchini; na
  8. Mwisho Ripoti inabainisha mafanikio, changamoto za sekta hii na njia ya kupata ufumbuzi.

>>Soma Zaidi>>