Home » images »

Matukio ya uzinduzi wa ripoti ya sekta ndogo ya petroli kwa mwaka 2016

 

Ripoti ya Sekta ndogo ya Petroli kwa mwaka 2016, ni ya tatu kutayarishwa na EWURA tangu ilipotoa ripoti ya kwanza ya mwaka 2014. Ripoti hizi hutolewa kila mwaka na zimekuwa zikiboreshwa mwaka hadi mwaka ili kukidhi mahitaji ya wadau mbalimbali. Ripoti hiyo imejumuisha takwimu muhimu na taarifa zingine kuhusiana na uendeshaji na hali ya biashara ya mafuta kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka 2016.

 

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Jamidu Kitima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Felix Ngamlagosi wakishuhudia uzinduzi wa Ripoti ya Sekta ndogo ya Petroli kwa mwaka 2016. Ripoti hiyo ilizinduliwa mjini Dodoma tarehe 19 Mei, 2017.

 

Meza kuu ikionesha Ripoti ya Sekta ndogo ya Petroli kwa mwaka 2016 baada ya kuzinduliwa. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Doto Biteko, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Jamidu Kitima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), Felix Ngamlagosi.