Nafasi za mafunzo ya ukataji vito kwa wanawake

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADININAFASI ZA MAFUNZO YA UKATAJI VITO KWA WANAWAKE

Kamati ndogo ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (Women Foundation Fund) iliyo chini ya kamati ya Maandilizi ya Arusha Gem Fair (AGF) inatangaza nafasi 18 za mafunzo ya muda mfupi katika fani ya ukataji na usanifu wa madini ya vito (Lapidary training course). Mafunzo hayo yatatolewa katika Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini, kilichoko eneo la Themi, jijini Arusha kuanzia mwezi Mei, 2017. Atakayechaguliwa kujiunga atalipiwa ada ya mafunzo hayo pekee. Hivyo muombaji atajitegemea kwa chakula pamoja na malazi kwa muda wote wa masomo.

Lengo la Mafunzo

Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha wanawake kujiajiri au kuajiriwa katika fani ya ukataji na usanifu madini ya vito ili kuongeza thamani ya madini hayo.

Muda wa Mafunzo

Muda wa mafunzo ya cheti cha Lapidary Technology utakuwa miezi sita (6).

Sifa za Muombaji

  • Awe mwanamke Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 30; na
  • Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea mwenye kufaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati.

Barua za maombi, CV na vyeti vitumwe kwa:-Mwenyekiti, Kamati ya AGF Women Foundation Fund, S.L.P 641, Arusha; au yaletwe kwa mkono katika ofisi za Madini Kanda ya Kaskazini zilizopo Themi,Njiro. Kwa maelekezo Zaidi piga simuNamba 027 254 4079. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/04/2017.