Taarifa kwa Umma-Dangote kupatiwa eneo la kuchimba makaa ya mawe lililopo Ngaka

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

 DANGOTE KUPATIWA ENEO LA KUCHIMBA MAKAA YA MAWE LILILOPO NGAKA

 Utaratibu wa kuipatia Kampuni ya Saruji ya Dangote eneo la kuchimba madini ya makaa ya mawe ili ichimbe yenyewe umekamilika leo tarehe 11 Machi, 2017. Kampuni hiyo itapewa leseni kwenye eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 9.98 katika eneo la Ngaka, Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.

Hii inatokana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilotoa tarehe 5 Machi 2017, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Mtwara. Katika ziara hiyo, Rais Magufuli aliiagiza Wizara ya Nishati na Madini kuipatia Kampuni ya Dangote, eneo lililopo Ngaka wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma ili wachimbe makaa hayo wao wenyewe kwa ajili ya uzalishaji wa saruji katika kiwanda hicho.

Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji katika sekta za Nishati na Madini ili kuhakikisha kuwa miradi mipya na iliyopo inachangia ipasavyo katika uchumi wa Taifa ili kutekeleza azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Imetolewa na Wizara ya Nishati na Madini

Machi 11, 2017