Taarifa kwa Umma-Kukaribisha maombi mapya ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Songwe

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

 KUKARIBISHA MAOMBI MAPYA YA LESENI ZA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI KATIKA MIKOA YA IRINGA, MBEYA NA SONGWE

Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi inakaribisha maombi mapya ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini kwenye maeneo yaliyoachwa wazi kutokana na kufutwa kwa maombi 1,168 ya leseni (PML) ambayo hayakulipiwa kwa muda mrefu. Aidha, kuna leseni  (PML) 101 ambazo zimefutwa kutokana na kushindwa kurekebisha makosa mbalimbali na maeneo hayo yako wazi kuanzia tarehe 13/02/2017. Orodha ya maombi na leseni zilizofutwa inapatikana kwenye ofisi za Madini Mbeya na Chunya; na pia itapatikana kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya zote za Mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe.

Maelekezo zaidi ya taratibu za kumiliki leseni za madini yanapatikana katika Ofisi za Madini na pia kwenye Tovuti ya Wizara ya Nishati na Madini: https://mem.go.tz/mineral-sector/

Imetolewa na;

Mhandisi John Nayopa

KAMISHNA MSAIDIZI WA MADINI

KANDA YA KUSINI MAGHARIBI

7 Machi, 2017

Click the following links to read more

    >>Application offer lapsed in South Western Zone>>

   >>Licenses cancelled in South Western Zone>>