Taarifa kwa Umma-Maonesho ya 6 ya kimataifa ya madini ya vito Arusha, trh 3-5 Mei 2017

 

Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wameandaa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito ya Arusha  (AGF), yatakayofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei, 2017 katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.

Maonesho hayo yanayotarajia kuwakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 1000 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito, yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kitovu cha Madini ya Vito Afrika. Pia, yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

>>Soma Zaidi>>