Taarifa kwa umma-Mhe. Profesa Muhongo amemteua Bw. Charles Abel Sabuni kuwa Mwenyekiti bodi ya TMAA

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Untitled

TAARIFA KWA UMMA

 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Bw. Charles Abel Sabuni, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

 Uteuzi huo ni wa muda wa miaka mitatu na umeanza tarehe 11 Oktoba, 2016 hadi tarehe 10 Oktoba, 2019.

 

Imetolewa na;

 

KATIBU MKUU

12 OKTOBA, 2016