Taarifa kwa Umma-Mnada wa pili wa kimataifa wa madini ya tanzanite wafanyika Jijini Arusha

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

 

TAARIFA KWA UMMA

MNADA WA PILI WA KIMATAIFA WA MADINI YA TANZANITE WAFANYIKA JIJINI ARUSHA

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imefanya Mnada wa pili wa kimataifa wa madini ghafi ya Tanzanite kuanzia tarehe 9 – 12 Februari 2017. Mnada huo umefanyika katika kituo cha Jemolojia (TGC) kilichopo jijini Arusha.

Kampuni tatu zinazochimba madini ya Tanzanite ambazo ni Tanzanite One Mining Company Ltd, Mathias J Lyatuu Mining na Tanzanite Africa Ltd; zilileta jumla ya gramu 990,444.04 za madini ghafi kwenye mnada huo kwa ajili ya mauzo.

Baada ya taratibu za mnada, jumla ya gramu 990,039.04 za Tanzanite ghafi ziliuzwa kwa Dola za Marekani 4,202,287.13. Hii ni sawa na 99.9% ya madini yote yalilyoletwa kwa ajili ya mauzo. Kutokana na mauzo hayo, Serikali inatarajia kukusanya mrabaha wa Dola za Marekani 210,114.36 sawa na Shilingi 466,453,871.43. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Simajiro inatarajia kulipwa Shilingi 27,987,232.29 kama Kodi ya Huduma.

Kampuni 68 kutoka nchi saba duniani ambazo ni Tanzania, Kenya, India, Sri Lanka, China, Uswisi na Ujerumani zimeshiriki katika mnada huo.

Imetolewa na:

 

KATIBU MKUU

Wizara ya Nishati na Madini

12/2/2017