Taarifa kwa Umma-Mradi wa Ngozi wa kuvuna nishati ya jotoardhi kwa ajili ya kuchoronga visima vya awali

 

Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) ilianzishwa Disemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongoza maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania. TGDC ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linalomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa 100%. Kampuni ilianza rasmi shughuli zake Julai, 2014 kwa jukumu na mamlaka ya kutafiti, kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi kwa uzalishaji umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.

TGDC inatarajia kuchoronga visima vya awali ikiwa ni hatua ya mwanzo katika kuvuna nishati ya jotoardhi. Hivyo uchambuzi wa athari za mazingira na jamii (ESIA) utafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 (Environmental Management Act Cap 191 of 2004) na kanuni zake za mwaka 2005 (Environmental Impact Assessment and Audit Regulations of 2005), lengo ni kuainisha faida lakini pia athari za mradi kabla ya utekelezaji.

>>Soma Zaidi>>