Taarifa kwa Umma-Ufafanuzi kuhusu Kampuni ya Mantra Tanzania kusitisha uchimbaji wa madini ya urani

 

Tarehe 9 Julai, 2017, magazeti ya The Guardian na The Citizen yaliandika habari  kuhusu Kampuni ya MANTRA Tanzania kusitisha (Suspension) uchimbaji wa Madini ya Urani (Uranium) kwenye leseni yao iliyoko eneo la Mto Mkuju sababu zikiwa ni kuporomoka kwa bei ya Urani katika Soko la Dunia pamoja na mabadiliko katika Sheria ya Madini.

Ieleweke kuwa, Kampuni ya Mantra Tanzania inayo leseni ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini (Special Mining Licence) SML NO. 489/2013 yenye eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 197.94 iliyotolewa tarehe 05/04/2013 na kabla ya Kampuni hiyo kuomba leseni ya uchimbaji madini ilifanya upembuzi yakinifu (feasibility study) na kuthibitisha kuwa kwa bei ya Urani ya wakati huo ambayo ilikuwa ni Dola za Marekani 65 kwa Ratili moja (US$ 65/Pound) hivyo mradi huo ungezalisha madini kwa faida.

Hata hivyo, bei ya Urani duniani ilianza kuporomoka na kufikia Dola 18.5 kwa ratili mwanzoni mwa mwaka 2017 na kwa sasa bei ni Dola 23 kwa ratili moja. Kufuatia kuporomoka huko kwa bei, Kampuni ilikokotoa gharama na kuonekana kuwa haiwezi kuzalisha urani kwa faida.

>>Soma Zaidi>>