Taarifa kwa Umma-Wakazi wa Mahenge na Lindi kulipwa fidia ya mradi wa madini ya graphite (kinywe)

 

Tarehe 4 Julai, 2017, gazeti la Mtanzania katika ukurasa wake wa viii, liliandika habari yenye kichwa cha habari “Miradi ya kinywe Nachingwea, Ulanga yalipa fidia,”.

Mwandishi wa habari husika alimnukuu aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini akisema kuwa “kwa kuzingatia umuhimu wa madini hayo, Serikali imeyapa kipaumbele na hivyo miradi ya Kinywe kule Mahenge na Lindi itaanza kutekelezwa na fidia imeanza kutolewa kwa wale wanaozunguka migodi tarajiwa kule Mahenge ambapo asilimia 80 ya waathirika wameshalipwa  vilivyo,”

Aidha, aliyekuwa Kaimu Kamishna wa Madini alinukuliwa akisema kuwa wananchi wote walioathirika na uchimbaji wa madini hayo wilayani Nachingwea wamekwishalipwa ili kupisha uanzishwaji wa shughuli ya uchimbaji wa madini hayo.

>>Soma Zaidi>>