Taarifa kwa vyombo vya habari-Ufafanuzi kuhusu mradi wa kusindika gesi asilia kimiminika (LNG)

 

Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mradi wa kusindika gesi asilia kimiminika (LNG), kufuatia taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la “The Guardian” la Tarehe 13 Februari, 2017, yenye kichwa cha habari “Tanzania LNG Project Stalls as Uncertainty rises-report”. Tafsiri ya kichwa cha habari inaonesha kwamba mradi umesimama, ama hatma yake haijulikani. Kichwa hiki cha habari hakina usahihi kwa kuwa mradi unaendelea vema, hatua mbalimbali za utekelezaji zimefikiwa na mipango ya utekelezaji inafahamika.

TPDC kama mbia katika mradi huu inapenda kutoa ufafanuzi na kueleza hatua mbalimbali za mradi zilizofikiwa hadi sasa.

>>Soma Zaidi>>