Tangazo kwa mara ya pili-Kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa kamati ya TEITI

 

Kifungu 7(2) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia, Mwaka 2015

Utangulizi

Utekelezaji wa shughuli za Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) zinasimamiwa na Kamati ya TEITI yenye wajumbe kumi na tano (15) kutoka makundi matatu:– Asasi za kiraia; Kampuni na Serikalini. Kila kundi linawakilishwa na wajumbe watano ambao uteuzi wao hufanywa kutoka katika makundi husika. Sheria tajwa hapo juu, imeweka utaratibu wa katika Kifungu cha 7 wa kumpata Mwenyekiti.

>>Soma Zaidi>>