Home » images »

Ujumbe wa Tanzania washiriki mkutano wa 36 wa SADC

 

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo unashiriki  Mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland.

Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano wa 36 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Swaziland, kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kolobelo.

Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Swaziland, Dkt. Sibusiso Dlamin umehudhuriwa na nchi mbalimbali ikiwemo  Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Swaziland, Botswana, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Botswana, Madagascar na Mauritius.

Masuala muhimu yaliyojadiliwa kwenye Mkutano husika ni pamoja na Mkataba wa Uanzishwaji wa Kituo cha Nishati Jadidifu na Matumizi bora ya Nishati (SADC Centre for Renewable Energy Efficiency-SACREE) na kuidhinisha Mpango wa Utekelezaji wa Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati.

Aidha mkutano huo pia ulijikita katika kujadili maendeleo ya udhibiti wa huduma za nishati katika nchi za SADC, maendeleo ya usambazaji mahitaji ya umeme, utekelezaji wa miradi ya kipaumbele pamoja na kuidhinisha Mpango wa kuelekea kwenye matumizi ya dizeli zenye kiwango kidogo cha sulphur.

Mkutano huo ulianza tarehe 8 Julai, 2017 na kumalizika tarehe 11 Julai, 2017.

Imeandaliwa na:

Teresia Mhagama,

Afisa Habari,

Wizara ya Nishati na Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

Barua Pepe: info@mem.go.tz,                                                                               

Tovuti: mem.go.tz