Home » images »

Uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa vituo na njia kuu ya kusafirisha umeme ya 132kv Mtwara-Lindi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vituo vya umeme vya msongo wa 132/33kv vyenye uwezo wa 20 MVA na Njia kuu ya kusafirisha umeme ya 132KV Mtwara- Lindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa vituo vya umeme vya msongo wa 132/33kv vyenye uwezo wa 20 MVA na Njia kuu ya kusafirisha umeme ya 132KV Mtwara- Lindi. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Tukio hili la Uwekaji jiwe la msingi lilifanyika Tarehe 5 Machi, 2017 na kushuhudiwa na viongozi waandamizi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wabunge wa Mkoani Mtwara, viongozi wa Mkoa wa Mtwara na viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mradi huu wa kusafirisha na kusambaza umeme wenye msongo wa kilovolti 132 utaondoa tatizo la umeme kuwa mdogo (low voltage) na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara  kwenye Mikoa  ya Mtwara na Lindi  kwani hapo awali hapakua na njia ya usafirishaji umeme ya Msongo wa Kilovolti 132, Zaidi ya njia za zamani za usambazaji umeme zilizopo zenye uwezo wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 33.

Imeandaliwa na:

Mohamed Saif,

Afisa Habari,

Wizara ya Nishati na Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606

Barua Pepe: info@mem.go.tz                                                                               

Tovuti: mem.go.tz